Maoni ya wahariri | Magazetini | DW | 07.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo pia wanatoa maoni juu ya vita vya Gaza.

Mjasiramali mkubwa wa Ujerumani Adolf Merckle aliejiua .

Mjasiramali mkubwa wa Ujerumani Adolf Merckle aliejiua .

Wahariri wa magazeti karibu yote ya Ujerumani leo pia wanazungumzia juu ya vita vya Gaza.

Wahariri hao , leo pia wanata maoni yao juu ya habari za kusikitisha, zinazomhusu tajiri mmoja mkubwa wa hapa nchini aliejiua ,Adolf Merckle

Juu ya vita vya Gaza mhariri wa gazeti la Nordwest anazungumzia hasa shambulio lililofanywa na Israel katika shule.Mhariri huyo anasema ,kuua raia wasiokuwa na njia yoyote ya kujihami ni jambo lisiloweza kusameheka asilani. Gazeti linatamka wazi kuwa shambulio hilo ni kitendo cha unyama na waliotoa amri, wanapaswa kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa .Lakini mhariri wa gazeti hilo pia anasema, haitakuwa sawa kuwasamehe wanaitikadi kali wa Hamas wanaofanya mashambulio ya roketi na kuua raia wa Israel wasiokuwa na hatia.

Juu ya masuala ya ndani magazeti ya Ujerumani yametoa maoni kuhusu mgogoro wa gesi, na juu ya kifo cha mjasiramali mkubwa wa hapa nchini, aliejiua. Kuhusu mgogoro wa gesi, magazeti karibu yote,katika maoni yao yanashauri ,kuchukuliwa hatua ili Ulaya magharibi iache kuitegemea Urusi kwa mahitaji yake ya gesi.

Na kuhusu mkasa wa tajiri mkubwa wa Ujerumani, Adolf Merckle aliekatiza maisha yake,gazeti la Schwäbische linasema mfanyabiashra huyo aliekuwa anafuata imani za jadi juu ya biashara, hakuweza kukubali kushindwa.Gazeti linasema,tofauti na wajasiriamali wa leo, wanaohamia kwengine, ikiwa wameshindwa mahala fulani, Adolf Merckle aliambatanisha maisha yake na kazi yake.Na gazeti la Pforzheimer linasema bilionea huyo alijiona kuwa alifikia mwisho, baada ya biashara yake kuenda mrama-kwani kwake, kazi na maisha, vilikuwa kitu kimoja.
 • Tarehe 07.01.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GTaD
 • Tarehe 07.01.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GTaD