Magazetini.
17 Septemba 2008Katika maoni yao, wahariri wa magazeti leo wanazungumzia juu ya bajeti ya Ujerumani kwa kipindi kijacho cha fedha.
Waziri wa fedha wa Ujerumani bwana Peer Steinbrück amewasilisha mswada wa bajeti ya Euro Bilioni 288.4 kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha. Maoni yanatofautiana juu ya bajeti hiyo.
Mhariri wa gazeti la Reutlinger General Anzeiger anatilia maanani kwamba bajeti hiyo imevunja rekodi. Kwani waziri wa fedha bwana Steinbrück ameongeza bajeti hiyo kwa Euro 5.2
Lakini mhariri anasema pia inapasa kutilia maanani vilevile kwamba ,katika mwaka ujao serikali kuu ya Ujerumani itapaswa kutenga kiasi cha Euro bilioni 42.5 kwa ajili ya kulipia riba.
Serikali ya Ujerumani inadaiwa jumla ya Euro bilioni 920.
Mhariri wa gazeti la Neue Osnabrücker
haoni afueni yoyote katika mswada wa
bajeti uliowasilishwa na waziri Steinbrück
japo lengo la waziri huyo wa fedha ni
kupunguza deni la serikali.
Gazeti hilo linatilia maanani kwamba wakati waziri huyo anataka kupunguza deni, matumizi yataongezeka kwa Euro bilioni 5.2 Mhariri wa gazeti anasema mambo hayo mawili hayawezi kuenda sambamba hasa wakati huu ambapo pana wasiwasi juu ya ustawi wa uchumi kutokana na mgogoro wa fedha nchini Marekani.
Gazeti la Schwäbische linasema lengo la kuwa na bajeti yenye urari lazima lifikiwe na wabunge wa vyama vyote vilivyomo katika serikali ya mseto, la sivyo hapatakuwa na sababu kwao , kuendelea kuwapo.
Mhariri wa gazeti hilo anawazungumzia wabunge wanaotaka kupunguza kodi badala ya kupunguza deni la serikali, bila ya kuzingtia ukweli kwamba deni la leo ndiyo kodi ya kesho.
Lakini mhariri wa gazeti la Mitteldeutsche anampongeza waziri wa fedha kwa kusema ukweli juu ya bajeti.
Gazeti linatilia maanani kuwa waziri huyo hakutoa ahadi zozote kwa wananchi alipowasilisha mswada wa bajeti. Mhariri anaeleza kuwa kuongezeka bei za nishati na chakula siyo mambo ya kupita,bali ni matokeo ya sera za dunia utandawazi. Bei ya nishati inapanda kutokana na ongezeko la mahitaji katika nchi kama China na Brazil- katika hali hiyo ruzuku za serikali hazitasaidia. Gazeti linasema hiyo ndiyo sababu kwamba waziri wa fedha bwana Steinbrück amepinga vikali wazo juu ya serikali kutoa ruzuku