Maoni ya wahariri. | Magazetini | DW | 05.08.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri.

Katika maoni yao wahariri wa magazeti ya Ujerumani pia wanazungumzia juu ya kifo cha mwandishi maaruf wa Urusi Alexander Solzhenitsyn.

Maombolezo ya Alexander Solschenizyn.

Maombolezo ya Alexander Solschenizyn.


Mwandishi maaruf wa Urusi Alexander Solzhenitsyn aliefichua udhalimu wa utawala wa Joseph Stalin katika Umoja wa Kisoviet amefariki. Katika maoni yao leo,wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumzia juu ya mwandishi huyo.

Wahariri wa magazeti leo pia wanazungumzia juu ya mkutano unaoendelea nchini Mexico ambapo wajumbe kutoka duniani kote wanajadili maradhi ya ukimwi , pia wanatoa maoni yao juu ya michezo ya olimpiki nchini China siku tatu tu kabla ya kufunguliwa mjini Beijing.


Juu ya kifo cha Alexander Solzhenitsyn gazeti la Lausitzer Rundschau linasema watu wanapaswa kumwomba radhi mwandishi huyo.

Mhariri anaeleza kuwa mwandishi huyo aliekuwa mshindi wa nishani ya Nobel katika fasihi mara nyingi hakusikilizwa iliyvopasa na mara nyingi hakueleweka. Gazeti linasema dunia ilipaswa kuzingatia kauli alizokuwa anatoa kutetea demokrasia na alizokuwa anatoa kupinga rushwa.

Gazeti la Badische Neueste Nachrichten pia limeandika juu ya kifo cha Alexander Solzhenitsyn, kwa kusema kuwa mwanaharakati huyo aliandika , pia kwa niaba ya wale ambao hawakuwa na majina katika Umoja wa Kisoviet.

Gazeti hilo linaeleza kuwa, ni wazi kwamba awali ya yote Solzhenitsyn aliandika juu ya uchungu uliokuwa rohoni mwake kuhusu mateso ya jela na ya wale aliokuwa karibu nao. Lakini iwapo mtu anasoma vitabu vyake kwa undani ataweza kubaini kwamba mwanaharakati huyo pia aliandika kwa niaba ya watu wote waliosibika chini ya utawala wa kigaidi wa Joseph Stalin katika Umoja wa Kisoviet. Mhariri wa gazeti la Badische Neueste Nachrichten anasema anatumai kwamba wanahistoria watazingtia urithi alioacha mwanaharakati huyo, hasa kutokana na kutambua kwamba uhalifu uliotendwa na Stalin katika kambi za Gulag bado haujashughulikiwa kwa ukamilifu.


Mhariri wa gazeti la Thüringische Landeszeitung anatupia macho maradhi ya ukimwi. Anasema katika maoni yake kuwa inawezekana kuwashughulikia watu wanaougua maradhi hayo .

Lakini mhariri huyo anaeleza kuwa siyo kila mgonjwa anaepata tiba. Bei ya dawa bado ni ya juu kwa wagonjwa wengi na hasa katika nchi zinazoendelea penye idadi kubwa ya wagonjwa.

Sababu ni kwamba mikakati ya kushughulikia maradhi hayo inadhibitiwa na watu wanaotetea maslahi fulani. Na kwa kadri inavyoendelea kuwa hivyo na ndivyo watu wananavyozidi kufa- maalfu kwa maalfu duniani kote.


Gazeti la Mannheimer Morgen linasema wakati zimebaki siku tatu kufanyika mashindano ya olimpiki,viongozi wa China wamezidi kuimarisha taratibu za ulinzi.

Gazeti linasema watawala wa China wanatumia mashambulio ya kigaidi kama mwao wa kukandamiza haki za binadamu.

Gazeti la Mannheimer linawaambia watu duniani wajitayarishe kuona michezo, sampuli ya mashindano ya olimpiki yaliyofanyika mjini Berlin mnamo mwaka 1936.

MODE:
Conlusion.

 • Tarehe 05.08.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EqnW
 • Tarehe 05.08.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EqnW