Maoni ya wahariri. | Magazetini | DW | 14.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Maoni ya wahariri.

Uchaguzi umefanyika katika jimbo la Bremen kaskazini mwa Ujerumani ambapo chama cha social demokratik kimeshinda . Lakini katika maoni yao leo wahariri wa magazeti wanasema kuwa washindi wa kweli ni wengine.

Chama cha Social Demokratik kimeshinda katika uchaguzi huo kwa kupata asilimia 38 ya kura kikifuatiwa na chama cha kansela Angela Merkel CDU kilichopata asilimia 25 ya kura. Lakini vyama hivyo ambavyo vimekuwa katika serikali ya mseto tokea mwaka wa 1995 katika jimbo hilo la Bremen jana vilipoteza

Juu ya uchaguzi huo mhariri wa gazeti la Heilbronner Stimme anasema kuwa washindi wa uchaguzi huo hasa ni chama cha kijani kilichonufaika kutokana na udhia wa mseto wa Berlin wa vyama vikubwa ,Social Demokratik na CDU.Na mshindi mwengine ni chama cha mlengo wa kushoto.

Mhariri huyo anasema matokeo ya uchaguzi huo yanathibitisha ulazima wa kufanyika mageuzi katika miundo ya majimbo. Anatamka kuwa wakati sasa umefika wa kupunguza mabunge ya majimbo.


Kutokana na matokeo ya uchaguzi huo gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linakipa chama cha Social Demokratik kwa kusema kuwa chama hicho kinapaswa kuondokana na mtanziko wa mseto mkubwa. Lazima sasa kitumie fursa hiyo ya nadra baada ya kushinda jana.Gazeti hilo linakitaka chama hicho kithibitishe kuwa inawezekana kujenga mseto unaoweza kufanya kazi.

Mhariri anaeleza kuwa baada ya miaka 12 ya serikali ya mseto baina ya chama hicho na chama cha CDU , na udhia mwingine baina yake na chama cha kijani , katika jimbo la Bremen sasa ,kimepata fursa nyingine ya kuonesha kuwa kinaweza kuenda pamoja na chama cha kijani.


Mhariri wa gazeti la MANNHEIMER MORGEN pia anazungumzia hayo hayo kwa kusema kuwa chama cha Social Demokratik kinapaswa kuunda mseto na chama cha kijani.

Mhariri huyo pia anatilia maanani udhia wa mseto mkubwa wa Berlin ambao anasema haubembei jinsi inavyotakikana. Anasema wapiga kura katika uchaguzi wa jana katika jimbo la Bremen walionyesha hayo katika kura zao.

Hivyo basi mhariri huyo pia anasema litakuwa jambo la busara ikiwa mshindi wa uchaguzi wa jana ,chama cha SPD kitaungana na chama cha kijani ili kuunda mseto.

Baadhi ya wahariri wanatathmini athari za matokeo ya uchaguzi wa jana kwa serikali kuu . Kwa mfano gazeti la MITTELBAYERISCHE ZEITUNG linasema katika maoni yake kuwa matokeo hayo takribani ni maafa kwa vyama vikuu.

Wahariri wengine wote wanasema katika maoni yao kwamba washindi halisi katika uchaguzi wa jana ni chama cha kijani kilichopata asilimia zaidi ya 16 na chama cha mlengo wa kushoto kilichopata asilimia zaidi ya nane ya kura.

Jambo wanalotilia maanani wahariri hao ni kuwa vyama vikuu vimepoteza kura katika uchaguzi huo kulinganisha na matokeo ya miaka ya nyuma.

Mhariri wa gazeti la SÜD-WEST PRESSE anasema matokeo ya uchaguzi wa jana siyo jambo la kufurahisha kwa mwenyekiti wa chama cha SPD bwana Kurt Beck, licha ya kujipa matumaini kwamba chama hicho kitaendelea kutawala kama anavyoeleza mhariri wa gazeti la Die ESSLINGER ZEITUNG.

AM.