Maoni ya wahariri juu ya mustakabal wa Ulaya | Magazetini | DW | 23.01.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya mustakabal wa Ulaya

Wahariri wanazungumzia juu ya mustakabal wa Ulaya katika muktadha wa uhusiano baina ya Ujerumani na Ufaransa na pia wanatoa maoni juu ya kodi ya miamala ya fedha

Waziri wa elimu wa Ujerumani Annette Schavan akabiliwa na tuhuma za kughushi tasnifu

Waziri wa elimu wa Ujerumani Annette Schavan akabiliwa na tuhuma za kughushi tasnifu

Gazeti la" Die Welt" linazungumzia juu ya mustakabal wa Ulaya. Mhariri wa gazeti hilo anasema bara la Ulaya limesimama mbele ya kizingiti cha aina mpya, na anaeleza kwa kuuelekeza ujumbe kwa Ujerumani na Ufaransa.

"Mbele ya bara la Ulaya kimesimama kiunzi." Mhariri wa gazeti hilo anasema Ujerumani na Ufaransa pia zitapaswa kukiruka kiunzi hicho. Anaeleza kuwa kinachohitajika ni sera mpya, na siyo kuendelea na tabia ya kusema mambo yanaweza kusonga mbele kama yalivyo.

Gazeti la"Stuttgarter"pia linauzungumzia mustakabal wa Ufaransa na Ujerumani kuhusiana na rika la vijana.Mhariri wa gazeti hilo anasema: maadamu, Ujerumani na Ufaransa haziwaonyeshi vijana wao njia ya kuleta matumaini ya siku za usoni, mwito juu ya kujenga urafiki utaishia katika ndoto." Spika wa bunge la Ufaransa ametoa ujumbe wa matumaini kwa vijana wote wa Ulaya.Lakini bado ni ujumbe tu.

Mhariri wa gazeti la "Neuen Osnabrücker" anashauri haja ya kuimarishwa kwa Umoja wa sarafu ya Euro kwa kusema kwa kusema kwamba changamoto zinazolikabili bara la Ulaya ni kubwa sana, na hivyo haziwezi kufunikwa na nderemo za maadhimisho. Mhariri huyo anasema bara la Ulaya linapaswa kuleta ufanisi katika umoja wa sarafu ya Euro sambamba na kuuimarisha umoja wa kisiasa.

Gazeti la "Stuttgarter Nachrichten" linasema katika maoni yake kwamba uongozi maana yake pia ni kuonyesha ishara kwa mabenki, kuwa nayo yanapaswa kuwajibika vile vile. Ndiyo sababu ni sahihi kabisa kuanzisha kodi ya mabenki. Mhariri wa gazeti hilo anafafanua; walanguzi wa hisa, wawekaji vitega uchumi na walariba, wote hao hawana budi kubeba sehemu ya mzigo. Lazima walipe kodi madhali wao ndiyo waliousababisha mgogoro mkubwa wa mabenki duniani.

Gazeti la "Stuttgarter Nachrichten" linasema athari za mgogoro waliousababisha bado zinaendelea kuwalemea hata wale wasiokuwa na hatia. ambo muhimu hapa ni haki. Kwani wakati wote ni mlipa kodi aliyelazimika kuingiza mkono mfukoni kulipa, pale ambapo mabenki yanashindwa kulipa.

Annette Schavan:

Kwa mara nyingine Waziri mwingine wa Ujerumani anakabiliwa na madai ya kugushi tasnisu ya uzamifu.Waziri huyo wa elimu, Annette Schavan,ni mshirika wa ndani wa Kansela Merkel.Juu ya madai hayo gazeti la "Straubinger Tagblatt" linasema" Mpaka sasa yametolewa madai dhidi ya madai juu ya waziri huyo". Lakini mhariri anaeleza hata ikiwa sehemu ya madai itabakia baada ya uchunguzi, sifa ya waziri huyo, pamoja na ya jumuiya yote ya elimu na sayansi itavurugika.

Mwandishi:Mtullya Abdu/ Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Josephat Charo