1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni juu ya kunyomgwa Saddam

30 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCex

WASHINGTON:

Kumekuwapo muitiko wa haraka juu ya kunyongwa kwa Saddam mapema asubuhi ya leo:Rais George Bush wa Marekani alikueleza kunyongwa kwa Saddam „ ni awamu muhimu katika historia ya Iraq“.

Waziri wa nje wa Uingereza,Margaret Beckett alisema kuwa, Saddam Hussein amewajibika kwa uhalifu alioutendea umma wa Iraq.

Mjini MOSCOW:

Urusi imeonya kwamba kunyongwa Saddam Hussein kunaweza kukachochea balaa kubwa nchini Iraq na ikaelezea masikitiko kuwa vilio vya kimataifa kuomba ahurumiwe havikusikilizwa.Russia,mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UM, ilipinga uvamizi uliongozwa na majeshi ya Marekani nchini Iraq.