Mandela awataka watu kuwajali wanaoishi na virusi vya ukimwi. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mandela awataka watu kuwajali wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Johannesburg. Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela amehutubia maelfu ya watu waliokusanyika kwa ajili ya tamasha la muziki kwa ajili ya siku ya ukimwi duniani mjini Johannesburgm, akitoa wito wa uwazi zaidi katika kujadili ugonjwa huo.

Rais wa Marekani George W. Bush pia ameadhimisha siku hiyo ya ukimwi kwa wito kwa wanasiasa watunga sheria kuidhinisha pendekezo lake la kupatiwa kiasi kingine cha dola bilioni 30 kwa ajili ya gharama za kupambana na ukimwi katika muda wa miaka mitano. Ametangaza mipango ya kuzuru bara la Afrika mapema mwaka ujao. Wanasiasa nchini Ujerumani wametahadharisha dhidi ya kuwa na matumaini makubwa katika vita dhidi ya ukimwi. Waziri wa maendeleo wa Ujerumani Heide – Marie Wieczorek-Zeul amesema ukimwi umeendelea kutishia jamii zote katika bara la Afrika. Zaidi ya watu milioni 30 duniani kote wameathirika na virusi ambavyo vinasababisha ukimwi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com