Magazetini: Baba Mtakatifu nchini Marekani | Magazetini | DW | 17.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Magazetini: Baba Mtakatifu nchini Marekani

Ziara ya Baba Mtakatifu nchini Marekani ikiwa ni tukio muhimu la kimataifa hii leo inazingatiwa pia na wahariri wa magazeti ya hapa Ujerumani.

Baba Mtakatifu Benedikt 16 akikaribishwa Marekani

Baba Mtakatifu Benedikt 16 akikaribishwa Marekani

Kwanza ni yaliyoandikwa na gazeti la “Kölnische Rundschau” kuhusu ziara hiyo:


“Kwenye ziara inabidi Papa Benedikt wa 16. ajihusishe kurekebisha sura ya kanisa lake ambalo msingi wake unazidi kuporomoka huko Marekani. Ya kwanza kuna kizazi kipya cha vijana ambao wanasema wanaamini lakini hawaendi kanisani, ya pili ni idadi ya wahamiaji kutoka Marekani ya Kusini ambao lazima yaunganishwe katika parishi na ya tatu waumini wengi miongoni mwa Wakatoliki Millioni 65 walioko Marekani wanakataa kufuata amri kutoka Vatikan. Na juu ya hayo kuna kashfa ya mapadre waliowaharibu watoto. Baba Mtakatifu alisema anaona aibu kubwa kuhusu ulegevu wa mapadre hao na kwamba atapiga vita njia yoyote ya kuwaharibu watoto katika kanisa. Suali lakini ni je, Baba Mtakatifu pia atayataja wazi kabisa masuala mengine magumu kama alivyofanya mwanzoni mwa ziara yake?”


Ni gazeti la “Kölnische Rundschau”. Na tubakie kidogo zaidi kwenye makala ya mhariri huyu ambaye anaangalia mbele kidogo katika ratiba ya ziara hiyo na anaendelea kusema hivi:


“Kutakuwa pia hotuba ya Baba Mtakatifu mbele ya Umoja wa Mataifa, hotuba ambayo lazima iwe ya kisiasa kama Benedikt 16. anataka kweli kusema kitu cha maana kuhusu masuala muhimu kama vita dhidi ya umaskini au mzozo wa Darfur. Na vilevile tusikilize vizuri yale atakayosema wakati atakapotembelea eneo la “Ground Zero” mjini New York ambalo ni kumbukumbu ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, mwaka 2001. Tusisahau kwamba viongozi wengine wa kanisa katoliki walilaumu Uislamu mkali.”


Uchambuzi mwingine kuhusu ziara ya Baba Mtakatifu nchini Marekani tunasoma katika gazeti la “Westfälische Nachrichten” ambalo linakumbusha siku Popu alipowasili Marekani. Limeandika:


“Ni vigumu sana kufahamu kwa nini Popu Benedikt 16. alikaribishwa Marekani siku ambapo mahakimu wa mahakama mkuu ya Marekani waliruhusu sindano ya sumu zitumiwe katika kutekeleza adhabu ya kifo. Ni kama pigo kwa wapinzani wa adhabu ya kifo wa kanisa katoliki. Hii inaonyesha wazi tofauti katika ya Marekani na Vatikan. Na tena ni pigo kwa Baba Mtakatifu ambaye katika hotuba yake ya kwanza alisisitiza dini iwe msingi wa siasa.”

 • Tarehe 17.04.2008
 • Mwandishi Dreyer, Maja
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DjZy
 • Tarehe 17.04.2008
 • Mwandishi Dreyer, Maja
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DjZy