1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Madereva wakubaliana na shirika la reli kuhusu mishahara

Bruce Amani
26 Machi 2024

Chama cha madereva wa matreni nchini Ujerumani - DGL kimesema kimefikia makubaliano ya mishahara na Shirika la Reli la Ujerumani - Deutsche Bahn.

https://p.dw.com/p/4e75n
Deutsche Bahn - ICE in Nahaufnahme
Migomo ya madereva wa treni Ujerumani ilivuruga shughuli za usafiri wa umma katika wiki za karibuniPicha: Micha Korb/picture alliance

Hatua hiyo imeumaliza mgogoro wa kikazi ambao ulisababisha migomo kadhaa na hata kufunguliwa kwa kesi mahakamani. DGL imesema kuwa maelezo zaidi yatatolewa katika kikao cha waandishi habari mjini Berlin Jumanne. Deutsche Bahn pia imesema itafanya mkutano na waandishi habari Jumanne mjini Berlin kuzungumzia hali ya sasa ya mazungumzo ya mishahara.

Soma pia: Madereva wa treni wa Ujerumani wagoma tena leo

Duru sita za mazungumzo, msururu wa migomo, mazungumzo yaliyoshindwa na kesi za mahakamani viliigubika hali hiyo ya kutoelewana katika miezi ya karibuni.

Migogoro mingine kadhaa ya kikazi, hasa inayohusisha viwanja vya ndege Ujerumani na shirika kubwa kabisa la ndege Ujerumani - Lufthansa, bado haijatatuliwa. Migogoro hiyo kwa pamoja ilivuruga shughuli za usafiri wa umma nchini Ujerumani katika wiki za karibuni hatua iliyosababisha ukosoaji mkubwa wa kisiasa na umma.