Machafuko yazuka mjini Mombasa baada ya sala ya Ijumaa | Habari za Ulimwengu | DW | 18.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Machafuko yazuka mjini Mombasa baada ya sala ya Ijumaa

Polisi nchini Kenya wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya mamia kadhaa ya waandamanaji wa kiislamu wanaopinga ushindi wa rais Mwai Kibaki katika uchaguzi wa Disemba 27 mwaka uliopita.

Maandamanao ya leo yamefanyika baada ya sala ya Ijumaa katika msikiti mkuu mjini humo katika siku ya tatu na ya mwisho ya maandamano yaliyoitishwa na upinzani lakini yakapigwa marufuku na polisi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com