Maandamano ya ‘No Kings’ yafanyika kupinga utawala wa Trump
29 Machi 2026
Matangazo
Waandaaji wamesema zaidi ya matukio elfu tatu yalipangwa, yakilenga sera za Trump kuhusu Iran, udhibiti wa uhamiaji, pamoja na kupanda kwa gharama ya maisha.
Katika mji wa St. Paul, waandamanaji walijaza uwanja wa bunge la jimbo la Minnesota, huku baadhi wakibeba bendera za Marekani zilizogeuzwa chini kama ishara ya kutoridhiswa.
Umati mkubwa pia ulikusanyika katika miji mikubwa kama New York, Los Angeles na Washington.
Ikulu ya White House imepuuza maandamano hayo, ikiyaita kazi ya mitandao ya kifedha ya mrengo wa kushoto, madai ambayo pia yameungwa mkono na baadhi ya wanasiasa wa chama cha Republican.
Hata hivyo, waandalizi wanasema harakati hiyo inaonyesha kuongezeka kwa kutoridhika miongoni mwa Wamarekani kote nchini.