LONDON:Maandamano ya kumwuunga mkono Aung San Suu Kyi leo | Habari za Ulimwengu | DW | 24.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Maandamano ya kumwuunga mkono Aung San Suu Kyi leo

Maandamano ya kupinga kuendelea kuwekwa mahabusu kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi nchini Mynmar yatafanyika katika miji kadhaa ikiwa pamoja na London, Berlin, Paris, Washington na Cape Town leo unapotimu mwaka wa 12 tokea mwanasiasa huyo awekwe mahabusu ya nyumbani.

Watu katika miji hiyo wataandamana mbele ya ofisi za ubalozi wa China.

China inahesabika miongoni mwa nchi zenye uzito mkubwa juu ya utawala wa kijeshi nchini Mynmar.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com