LONDON : Leo ni Maadamano ya Siku ya Dafur | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Leo ni Maadamano ya Siku ya Dafur

Maandamano ya kuadhimisha Siku ya Dafur duniani yanapangwa kufanyika duniani kote leo hii kudai kukomeshwa kwa vitendo vya ubakaji wa wanawake na wasichana kwa mkururo katika jimbo la Dafur nchini Sudan.

Waandamanaji wa kike wanatazamiwa kupiga vin’gora vya tahadhari na kupuliza vifilimbi katika ofisi za ubalozi wa Sudan mjini London na katika miji mengine mikubwa duniani.

Katika baruwa ilioachapishwa katika mkesha wa kuamkia siku ya mandamano hayo yaliopangwa kufanyika leo hii wanawake kadhaa mashuhuri wanaoheshimika wametowa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukuwa hatua hivi sasa kukomesha ubakaji na ukatili wa kingono unaotumika kama silaha ya vita katika maisha ya kila siku.

Inaaminika kwamba vitendo hivyo hufanywa na wanajeshi wa Sudan na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Sudan.

Zaidi ya watu 200,000 wameuwawa huko Dafur na wengine milioni mbili na nusu wamepotezewa makaazi yao katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com