1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ligi ya Ujerumani kuanza tena Mei 16

Daniel Gakuba
7 Mei 2020

Msimu wa ligi ya Ujerumani-Bundesliga utaanza tena Mei 16, kwa kuchezwa pasipo mashabiki uwanjani, ikiwa ni takribani miezi miwili tangu usimamishwe kutokana na janga la virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3buak
Fussball, Bundesliga | Borussia Mönchengladbach - 1. FC Köln
Picha: picture-alliance/dpa/Fotostand

Tangazo hilo la leo linatolewa siku moja tu, baada ya vilabu vya kandanda kuambiwa msimu unaweza kuanza kutokana na mkutano wa Kansela Angela Merkel na viongozi wa majimbo 16 ya Ujerumani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Ligi ya Soka ya Ujerumani Christian Seifert amesema uamuzi huo una maanisha uhai wa uchumi wa vilabu.

Na kwamba kila mtu anapaswa kuwa macho kabisa kwamba ni michezo ya majaribio na kusisitiza kila mmoja kusimamia vyema majukumuku yake.

Siku ya mwazo Jumamosi ya Mei 16 mchuano huo utazikutanisha timu 12 ambapo  Borussia Dortmund itafuana na Schalke, Leipzig  na Freiburg, Hoffenheim na Hertha Berlin, Dusseldorf na Paderborn  na Augsburg  na  Wolfsburg.