Kwa ajili ya ukuaji wa uchumi na mapambano dhidi ya mzozo wa kiuchumi, Wen Jiabao yu pamoja na Ujerumani. | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kwa ajili ya ukuaji wa uchumi na mapambano dhidi ya mzozo wa kiuchumi, Wen Jiabao yu pamoja na Ujerumani.

Waziri mkuu wa China Wen Jiabao asisitiza hali ya kuaminiana katika ziara yake ya bara la Ulaya.

default

Kansela wa Ujeruman Angela Merkel, akimsalimu siku ya Alhamis , 29. Januar 2009, waziri mkuu wa China, Wen Jiabao,na kumkaribisha katika ofisi ya kansela mjini Berlin.


Katika ziara ambayo ni ya kujenga hali ya kuaminiana, waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, ameisisitiza hali hiyo katika ziara yake ya hivi sasa katika bara la Ulaya. Katika kituo chake cha pili cha ziara hiyo, mjini Berlin jana Alhamis Wen hakuivuruga hali hiyo. Ameleta hali ya kupatana zaidi.

Katika mtazamo kuhusiana na mzozo wa kifedha na kiuchumi duniani, nchi hizi mbili zinalenga kuimarisha ushirikiano wao wa pamoja.Wen Jiabao alikuwapo mjini Berlin kwa muda wa saa 20 tu. Kiongozi huyo wa China, hata hivyo, alihitaji saa sita katika mazungumzo yake na kansela Angela Merkel. Suala lililochukua nafasi ya juu kabisa ikiwa ni kuaminiana, wakanywa chai katika ofisi ya kansela, ikiwa ni ishara ya urafiki, takrima ambayo hupewa baadhi tu ya wageni.

Ujerumani itamshawishi waziri mkuu huyo wa China, kama alivyohakikisha waziri wa uchumi wa Ujerumani, Michael Glos, kuwa Ujerumani iko wazi kununua dhamana za akiba ya fedha za serikali kutoka China. Waziri wa sheria wa Ujerumani, Brigitte Zypries, ameisifu China kuwa ni nchi inayoelekea katika taifa linaloheshimu sheria, licha ya kuwa mwelekeo huo inafahamika kuwa bado uko mbali.

Na hata chama cha Green , ambacho kina msimamo mkali katika kupigania haki za binadamu kimeridhia katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa China, kama alivyosema mwanasiasa anayehusika na masuala ya kigeni katika chama cha Green, Jürgen Trittin , tunanukuu , kama vile mwalimu anavyomuelekeza mwanafunzi kuhusu makosa yake, mapungufu katika haki za binadamu ni kosa nchini China kama vile ilivyo kosa kuinyamazia hali hiyo, mwisho wa kunukuu.


Na hayo ndio pia mawazo ya kansela. Amemshauri mgeni wake huyo kutoka China kuwa na mazungumzo na Dalai Lama na kutoa pendekezo kuwa Ujerumani itakuwa mpatanishi. Mbali ya hayo, lakini, hali ya kukaribiana ilionekana. China ikajibu kwa kueleza kuwa Ujerumani itakuwa mshirika muhimu kutoka Umoja wa Ulaya. Mvutano kutokana na ziara ya Dalai Lama , kiongozi wa kidini wa jimbo linalotaka kujitenga la Tibet katika ofisi ya kansela, unaonekana kusahaulika. Mbinyo wa mzozo wa kifedha na kiuchumi duniani umesababisha mataifa haya mawili ambayo ni wasafirishaji wakubwa wa bidhaa nchi za nchi duniani kujiweka pamoja. Mataifa yote haya, lakini, hayafahamu hali ya masoko ya nje kwa sasa. Na hali hiyo kwa hivi sasa inaingiliana. Kwa serikali ya China, hali hiyo ni hatari zaidi kuliko kwa upande wa Ujerumani. China inahitaji ukuaji wa uchumi kwa takriban asilimia nane, na hii pekee ndio sababu inajaribu kuweka msukumo zaidi katika kupata nafasi zaidi za ajira kadri inavyowezekana.

Ukosefu wa nafasi za kazi unahatarisha uthabiti wa kijamii nchini China, pamoja na mamlaka ya chama cha kikomunist nchini China.


Sekione Kitojo/ ZR.

►◄
 • Tarehe 30.01.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GjsH
 • Tarehe 30.01.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GjsH
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com