1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuvamia Reichstag:Shambulio la moyo wa demokrasia Ujerumani

Sekione Kitojo
30 Agosti 2020

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameshutumu vikali waandamanaji walioandamana kupinga masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona waliovamia jengo la bunge Reichtag mjini Berlin Jumamosi (29.08.2020).

https://p.dw.com/p/3hlb6
Deutschland Berlin Protest gegen Corona-Maßnahmen
Picha: Reuters/A. Schmidt

 "Vurugu zilizotokea  za  bendera  za  Reich  na wenye msimamo mkali wa  mrengo  wa  kulia mbele  ya  jengo  la  bunge  la  Ujerumani ni shambulio  ambalo  haliwezi  kuvumilika  katika  moyo wa demokrasia  yetu. Hatutakubali hali  hiyo," Steinmeier  alisema leo Jumapili (30.08.2020).

Deutschland Berlin Protest gegen Corona-Maßnahmen
Vurugu katika ngazi za kuingia katika jengo la bunge mjini BerlinPicha: Reuters/C. Mang

Bendera  yenye  rangi  nyeusi, nyeupe  na  nyekundu, bendera ya kihistoria ya  Ujerumani  ya  enzi  za  Reich, ama  himaya, mara kadhaa  hutumiwa na watu wenye  msimamo  mkali  wa  mrengo  wa kulia  wa  siku  hizi.

"Demokrasia yetu iko  hai," Steimeier  alisema.

Mtu yeyote ambaye ana  hasira  juu  ya  hatua  zinazochukuliwa  na Ujerumani  kudhibiti virusi  vya  corona  au  ana  shaka na  umuhimu wake  anaweza  kujieleza, hata  katika eneo la  umma, hata  kwa maandamano , alisema.

"Kuelewa kwangu kunafikia  kikomo wakati  waandamanaji wanakubali  kuingizwa  katika  mkumbo wa  maadui  wa  demokrasia pamoja  na  wanaohamasisha masuala ya  kisiasa."

Deutschland Berlin Protest gegen Corona-Maßnahmen
Muandamanaji akiwa na bango lililoandikwa "acheni uongo wa corona"Picha: Reuters/C. Mang

Steinmeier  aliwashukuru  maafisa wa  polisi,"  "ambao walichukua hatua kali katika  mazingira  magumu."

Wavamia bunge

Jumamosi jioni, waandamanaji  wanaopinga  sera za kudhibiti  virusi vya  corona  nchini  Ujerumani walivunja  vizuwizi katika  jengo  la bunge Reichtag, ambalo ni  jengo  la  bunge  la  Ujerumani  katikati ya  mji  wa  Berlin, na  kuvamia  wakiingia  hadi  katika  ngazi  za kuingilia  katika   jengo  hilo.

Maafisa wa  polisi  waliwasukuma  nyuma  na  kuwapulizia  gesi  ya pilipili. Kulikuwa  na  mapambano.

Hapo  kabla  kulikuwa  na  maandamano  katika  jengo  la  bunge la Reichtag.

Deutschland Berlin Protest gegen Corona-Maßnahmen
Maafisa wa polisi wakiwadhibiti waandamanaji mjini BerlinPicha: Reuters/A. Schmidt

Bendera za rangi nyeusi, nyeupe  na  nyekundu  za  himaya  hiyo  ya kifalme  inayotumiwa  na  kile  kinachoitwa (wananchi  wa himaya hiyo) ambao ni  kundi lenye msimamo mkali pia zilikuwapo.

Kiasi ya  watu  38,000 walishiriki  katika  maandamano  hayo  dhidi ya  vizuwizi  vya  corona mjini  Berlin siku  ya  Jumamosi licha  ya juhudi  za  polisi kuwatawanya kutokana  na  kitisho cha kuambukizana  virusi  vya  corona.