Kura ya maoni kuhusu katiba Kenya kufanyika kesho | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.08.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Kura ya maoni kuhusu katiba Kenya kufanyika kesho

Usalama umeimarishwa kote nchini Kenya hasa katika maeneo yaliyo ngome ya wafuasi wanaoipinga katiba mpya

Usalama umeimarishwa kuzuia kutokea machafuko kama haya ya baada ya uchaguzi wa 2007

Usalama umeimarishwa kuzuia kutokea machafuko kama haya ya baada ya uchaguzi wa 2007

Kenya inajiandaa kuipigia kura ya maoni rasimu ya katiba mpya hapo kesho Jumatano.Usalama umeimarishwa kote nchini humo hasa katika maeneo ya Mkoa wa Bonde la Ufa ambako kulizuka ghasia baada ya uchaguzi mkuu wa Disemba mwaka 2007.Katiba hiyo mpya ni sehemu ya mageuzi ya kisiasa yaliyo na azma ya kuzuwia ghasia kutokea wakati wa uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika mwaka 2012.

Shughuli nzima itasimamiwa na kiasi ya waangalizi zaidi ya alfu moja wa Jumuiya ya Madola,Commonwealth na Shirika la maendeleo ya Kikanda,IGAD.Kwa mara ya kwanza, matokeo ya kura hiyo yatatangazwa kutumia huduma za mtandao na simu za mkononi.

Ili kupata sura kamili ya maandalizi hayo mwandishi wetu wa Nairobi Alfred Kiti ametuandalia ripoti ifuatayo.

Mtayarishaji:Alfred Kiti

Mpitiaji:Thelma Mwadzaya

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

 • Tarehe 03.08.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Oani
 • Tarehe 03.08.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Oani
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com