Kuondolewa kwa mkuu wa kikosi cha Polisi nchini Kenya | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.09.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kuondolewa kwa mkuu wa kikosi cha Polisi nchini Kenya

Hisia na maoni mbali mbali yamejitokeza kufuatia kuondolewa kwa Mkuu wa Kikosi cha Polisi nchini Kenya Meja Jenerali Hussein Ali.

default

Rais Mwai Kibaki amefanya mabadiliko katika kikosi cha Polisi

Meja Jenerali Ali ameteuliwa kuwa Msimamizi Mkuu wa Shirika la Posta nchini Kenya na nafasi yake kuchukuliwa na Mathew Kirai Iteere aliyekuwa kamanda wa kikosi cha polisi wa kupambana na ghasia – GSU.

Ali ambaye alikuwa katika wadhifa huo wa ukuu wa polisi kwa muda wa miaka sita amekumbana na changamoto nyingi zikiwemo kukabiliana na kundi haramu la Mungiki, sifa mbaya ya kikosi cha polisi na tuhuma za kikosi hicho kuhusika katika mauaji ya kiholela. Shutuma kuu aliyoipata ni kushindwa kuzuia machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu mwanzoni mwa mwaka uliopita.

Kutoka Nairobi Alfred Kiti ametutumia taarifa ifuatayo...

Imetayarishwa na  Alfred Kiti

Mpitiaji:Aboubakary Liongo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com