1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Hali ya utulivu imerejea baada ya mapambano ya siku moja

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtR

Vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya vimeimarisha usalama katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Hali ya utulivu imerejea mjini Kinshasa,siku moja baada ya mapambano kuzuka kati ya wafuasi wa wagombea wadhifa wa urais na kusababisha vifo vya watu wanne.Mapambano hayo yalitokea karibu na nyumba ya makamu wa rais Jean-Pierre Bemba aliekabiliana na rais wa hivi sasa Joseph Kabila,katika duru ya pili ya uchaguzi tarehe 29 mwezi wa Oktoba.Sehemu ya matokeo ya uchaguzi iliyochapishwa na halmashauri ya uchaguzi ya nchi hiyo na kutayarishwa na wanadiplomasia,huonyesha kuwa Kabila anaongoza.Wafuasi wa Bemba wanatuhumu wana ushahidi kuwa kumefanywa udanganyifu wa mpangilio katika utaratibu wa kuhesabu kura.