1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un: Ziara ya Urusi inaonyesha umuhimu wa kimkakati

13 Septemba 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema ziara yake nchini Urusi inaonyesha "umuhimu wa kimkakati" wa uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4WGV9
Bildkombo I Wladimir Putin und Kim Jong Un
Picha: Mikhail Klimentyev/Sputnik, Kremlin/Korean Central News Agency/AP/picture alliance

Kim anatarajiwa siku ya Jumatano kushiriki mkutano wa kilele na  Rais Vladimir Putin wa Urusi. Mkutano huo unafuatiliwa kwa karibu na Marekani pamoja na washirika wake, ambao wana wasiwasi kuwa viongozi hao wawili watajadili ushirikiano wa kijeshi na huenda wakakubaliana juu ya mpango wa biashara ya silaha na teknolojia ya ulinzi.

Marekani na Korea Kusini zimeonya juu ya biashara yoyote ya silaha na Korea Kaskazini na kusema itakuwa ni ukiukaji wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambayo Urusi iliyaidhinisha.