Kiev. Kumbukumbu ya Chernobyl leo. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kiev. Kumbukumbu ya Chernobyl leo.

Watu nchini Ukraine, Russia na Belarus wanaadhimisha miaka 21 tangu mkasa wa maafa ya kinu cha kinuklia cha Chernobyl.

Mjini Kiev, rais wa Ukraine Viktor Yushchenko aliweka shada la maua kwa kumbukumbu ya wahanga.

Kulipuka kwa kinu hicho mwaka 1986 kulisambaza miale ya sumu katika eneo kubwa la Urusi ya zamani pamoja na Ulaya ya kaskazini.

Tukio ambalo lilisababisha watu wanaokadiriwa kufikia 500 kuwawa mara moja.

Katika muda mrefu, shirika la afya la umoja wa mataifa limeweka idadi ya watu waliofariki kutokana na tukio hilo kuwa 4,000.

Kwa jumla watu 300,000 waliondolewa kutoka katika maeneo yao ya miji na vijiji. Kiasi cha watoto 5,000 wamekutikana na kansa ya thyroid , ambayo huonekana katika koo.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameitaka jumuiya ya kitaifa kuanzisha tena msaada wao , ikiwa ni pamoja na msaada wa maendeleo ya kijamii, kwa maeneo yaliyoathirika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com