1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Keir Starmer asaini mikataba kadhaa akiwa China

29 Januari 2026

Ziara ya waziri mkuu Keir Starmer Beijing imeafikia mikataba kadhaa yenye maslahi ya kiuchumi kwa London

https://p.dw.com/p/57hlo
Waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer
Waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer Picha: Vincent Thian/REUTERS

Waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesifu hatua iliyopigwa kati ya nchi yake na China kuhusu masuala kadhaa ikiwamo ushuru na kuondolewa kwa visa za kuingia China kwa raia wa nchi yake.

Starmer amemwambia rais Xi Jinping mjini Beijing kwamba, China ni mdau muhimu katika jukwaa la dunia na kwa hivyo wanabidi kujenga mahusiano ya kipekee ya ushirikiano na Uingereza.

Starmer azuru China kurekebisha uhusiano na kusaka fursa za biashara

China kwa upande mwingine imetilia mkazo haja ya kuweko ushirikiano thabiti utakaozingatia mwelekeo wa muda mrefu kutokana na hali ya kimataifa inayobadilika.

Starmer, ambaye ziara yake China inamalizika Jumamosi, ametia saini pia mikataba kadhaa ya ushirikiano baada ya kukutana na waziri mkuu Li Qiang mjini Beijing.