1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Mapigano makali kusini mwa Afghanistan

7 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSB

Eneo la kusini mwa Afghanistan,linashuhudia mapigano makali kabisa tangu nchi hiyo kuvamiwa chini ya uongozi wa Marekani katika mwaka 2001.Siku ya Alkhamisi,wanajeshi 2 wa NATO waliuawa katika miripuko mbali mbali ya bomu. Kwa mujibu wa maafisa wa Kimarekani,zaidi ya wanamgambo 20 waliuawa katika mapigano yaliyozuka kwenye jimbo la Kandahar,kusini mwa Afghanistan, baada ya wanamgambo darzeni kadhaa,kushambulia vikosi vilivyokuwa vikipiga doria.Hapo awali, vikosi vya ushirikiano viliripoti kuwa zaidi ya wapiganaji 40 wa Taliban waliuawa siku ya Jumatano katika mapigano yaliyozuka Shah Wali Kot,jimboni Kandahar.