1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaua wapiganaji 40 kwenye mahandaki ya Gaza

1 Desemba 2025

Jeshi la Israeli jana Jumapili limesema limewaua zaidi ya wapiganaji 40 wa Kipalestina katika operesheni zilizolenga mitandao ya mahandaki karibu na Rafah, Ukanda wa Gaza, wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/54WlA
Israel - Militäroperation in Rafah
Israel - Militäroperation in RafahPicha: Israeli Army/REUTERS

Makumi ya wapiganaji wa Hamas wamejificha kwenye mahandaki ya kusini mwa Gaza, chini ya maeneo yanayodhibitiwa na jeshi la Israeli. Kwa siku 40 zilizopita, wanajeshi wamekuwa wakilenga juhudi zao mashariki mwa Rafah, kwa lengo la kuvunja njia za mahandaki zilizobaki katika eneo hilo na kuwaangamiza wanaojificha humo.Vyanzo kadhaa vilivyozungumza na  AFP siku ya Alhamisi vimesema kuwa kuwa mazungumzo yanaendelea kuhusu hatima ya wapiganaji waliobaki kwenye mtandao wa handaki kusini mwa Gaza. Na Jumatano, Hamas ilizitaka nchi zinazoshiriki mazungumzo zishinikize Israel kuwaruhusu wapate njia salama ikiwa ni mara ya kwanza kundi hilo la kukiri hadharani hali hiyo.