Israel yafunga vivuko vya mpakani | Habari za Ulimwengu | DW | 18.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Israel yafunga vivuko vya mpakani

Waziri wa ulinzi wa Israel, Ehud Brak, ameamuru vivuko vya mpakani kuingia Gaza vifungwe kwa muda. Hatua hii mpya ni pigo kubwa kwa usafirishaji wa chakula na bidhaa muhimu zinazohitajika katika eneo la Ukanda wa Gaza huku miji ya Israel iliyo karibu na Gaza ikiednelea kushambuliwa kwa maroketi.

Uamuzi wa waziri wa ulinzi wa Israel unanuia kuwashinikiza viongozi wa chama cha Hamas wakomeshe mashambulizi ya maroketi kusini mwa Israel.

Mwanamgambo mmoja wa kipalestina ameuwawwa na watu wengine wanne wakajeruhiwa katika uvamizi wa jeshi la Israel uliofanywa leo katiak Ukanda wa Gaza.

Shirika la Umoja wa Mataifa linawahudumia wakimbizi wa kipalestina leo limeitolea mwito Israel ivifungue vivuko vyote vya mpakani kwenda Gaza ambako wakaazi wote wa eneo hilo wanategemea misaada ya chakula.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com