1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na miaka 60 tangu kuundwa taifa hilo

8 Mei 2008
https://p.dw.com/p/DwW7

Jerusalem.

Sherehe kubwa inafanyika nchini Israel leo sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuundwa taiafa hilo la Kiyahudi, siku ambayo itaadhimishwa rasmi Jumatano ijayo. Sherehe hizo ziligubikwa na maonyesho ya ndege za kivita angani. Pamoja na hayo majeshi ya usalama yamewekwa hatika hali ya tahadhari, pakihofiwa hujuma za wanaharakati wa kipalestina. Maafisa wameyafunga maeneo ya kutoka na kuingia ukingo wa magharibi. Aidha zinafanyika katika wakati ambao Waziri mkuu Ehud Olmert akiandamwa na uchunguzi ju ya ufisadi , huku hatima yake ya kisiasa ikiwa mashakani. Israel inaadhimisha miaka 60 ya kuundwa dola hiyo, wakati bado haijafikia amani na wapalestina wanapigania pia kuwa na taifa lao.