ISLAMABAD:Rais Musharraf kuachia madaraka ya kijeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 17.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Rais Musharraf kuachia madaraka ya kijeshi

Rais Pervez Musharaf wa Pakistan anapanga kuachia madaraka ya kijeshi kufikia tarehe 15 mwezi Novemba.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye chama kinacho tawala cha Pakistan Muslim League, katibu mkuu wa chama hicho Mushahid Hussain Sayed amesema kuwa jenerali Musharraf atajiuzulu wadhfa wake wa kijeshi baada ya uchaguzi wa rais.

Jenerali Musharraf anatarajia kutetea tena kiti cha rais pindi muda wake utakapomalizika kati kati ya mwezi Oktoba.

Mahakama ya nchini Pakistan inajadili iwapo kiongozi huyo ana haki ya kuendelea kuwa na cheo cha juu cha kijeshi ikiwa anataka kugombea tena urais.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com