Iran yashambuliwa na Israel na Marekani
7 Aprili 2026
Maafisa wa Iran wamesema wimbi la mashambulio makali ya anga yaliyofanywa na Marekani na Israel yamefanya uharibifu kwenye madaraja kiasi mawili,miundo mbinu ya reli na barabara kuu leo Jumanne.
Shirika la habari la Iran limeripoti mashambulio yaliyofanywa dhidi ya daraja moja karibu na mji mtakatifu wa Qom na dhidi ya njia ya reli ya mji wa Kashan ambako watu wawili wameuliwa na watatu kujeruhiwa.
Uingereza yaongoza mkutano wa kujadili kufunguliwa kwa Hormuz
Mashambulio hayo ambayo pia yamethibitishwa na waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu, yamefanywa saa chache kabla ya muda wa mwisho uliotolewa na rais Donald Trump wa kuilazimisha Iran ifungue mlango bahari wa Hormuz.
Tehran nayo imeshambulia kiwanda cha kemikali ya kuchakata mafuta na gesi nchini Saudi Arabia. Qatar kwa upande mwingine imeonya kwamba vita vya Mashariki ya kati viko katika mwelekeo wa kutodhibitika tena kufuatia kitisho kilichotolewa na rais Trump cha kuishambulia miundo mbinu yote ya Iran.