1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakana kuhusika na kuvishambulia vikosi vya Marekani

5 Desemba 2023

Mjumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa Amir Saeid Iravani amesema nchi yake haijahusika katika matukio yoyote ya kushambulia vikosi vya Marekani.

https://p.dw.com/p/4ZnK0
Iran Soldaten
Jeshi la Iikiwa katika mazoezi ya kila mwaka ya kijeshi katika eneo la fukwe la IranPicha: Iranian Army/WANA/REUTERS

Tamko hilo laIran limechapishwa na shirika la habari linalomilikiwa kwa sehemu na serikali, la Tasnim leo Jumanne, na limekuja baada ya hapo jana mshauri wa Marekani kuhusu masuala ya usalama, Jake Sullivan, kuwaambia waandishi habari kwamba, Marekani inayo kila sababu ya kuamini kwamba mashambulio yanayoshuhudiwa katika eneo la bahari katika mashariki ya kati yanaihusisha Iran. Sullivan alisema mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Kihouthi kutoka Yemen dhidi ya meli kadhaa ikiwemo tatu za kibiashara hivi karibuni katika bahari ya Shamu yameungwa mkono kikamilifu na Iran. Tangu vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas vilipozuka Oktoba 7, yameshuhudiwa matukio kadhaa ya kushambuliwa kwa meli za kigeni katika eneo la bahari  la mashariki ya kati ambayo Marekani imedai yamekuwa yakifanywa na waasi wa Kihouthi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW