1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Raisi hakuhudhuria mkutano wa Erdogan Uturuki

28 Novemba 2023

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amekosa kuhudhuria mkutano wa kilele mjini Ankara, Uturuki ambao Rais Recep Tayyip Erdogan aliutangaza kwa waandishi wa habari.

https://p.dw.com/p/4ZY1V
Rais wa Iran Ebrahim Raisi
Rais wa Iran Ebrahim RaisiPicha: Iranian Presidency/dpa/picture alliance

Hata hivyo, Iran haikuthibitisha rasmi iwapo rais wake angehudhuria mkutano huo au la.

Ofisi ya rais wa Uturuki imeliambia shirika la habari la AFP kuwa, Erdogan hakupangiwa kufanya mkutano leo na haikutoa ufafanuzi iwapo ziara ya Ebrahim Raisi ilikuwa imefutwa au imeahirishwa.

Soma pia:Iran yapinga mahusiano kati ya Israel na mataifa ya kiarabu

Mkanganyiko juu ya ziara hiyo unaonyesha mvutano uliopo kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu kubwa za kikanda licha ya Iran na Uturuki kuwa na msimamo wa pamoja kuhusu mzozo kati ya Israel na Hamas.

Erdogan alitangaza mapema mwezi huu kuwa rais wa Iran Ebrahim Raisi ataizuru Uturuki mwisho mwa mwezi Novemba ili kufanya mazungumzo huu ya kinachoendelea katika ukanda wa Gaza.