1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani ataka mageuzi yasonge mbele.

Mtullya, Abdu Said17 Juni 2008

Rais wa Ujerumani Horst Köhler amewataka wajerumani wasonge mbele na maguezi yaliyoleta mafanikio katika sekta ya ajira vilevile.

https://p.dw.com/p/ELnR
Rais Horst Köhler wa Ujerumani.Picha: picture-alliance/ dpa


Rais Horst Köhler wa Ujerumani  ametoa mwito juu  ya  kusonga  mbele na mageuzi  yaliyoleta ustawi  wa uchumi na nafasi  za  ajira nchini  Ujerumaji.

Rais  Köhler amesema hayo katika hotuba aliyotoa  mjini Berlin leo.

Rais  Köhler pia amewataka wajerumani wabuni ajenda ya mwaka 2020 ili kufuatilia ajenda ya mageuzi iliyopitishwa chini ya uongozi  wa Kansela wa hapo  awali  Gerhard Schröder  iliyokabiliwa na  upinzani mkali.

Rais  Köhler amesema  ajenda ya mageuzi imeleta  mafanikio katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Kutokana  na mageuzi  hayo  watu  zaidi  ya  milioni moja na  laki sita  wamerejea  kazini ikiwapamoja  na wale ambao  kwa muda mrefu  hawakuweza  kupata ajira  kwa muda  mrefu  kutokana na umri wao mkubwa.

Juu ya elimu kiongozi huyo  wa Ujerumani  amesema  Ujerumani inahitaji kujenga mazingira  ambapo elimu itatambulika. Amewataka wajerumani  wajenge nchi inayoheshimu elimu- nchi ambapo wanaofanya juhudi za kutafuta elimu wanaheshimiwa. Amesisitiza umuhimu wa kuleta utengemano wa  kijamii baina ya  wananchi  wote . Ameeleza  kuwa utengemano  huo pia unapaswa kuhimizwa baina ya  vijana  na wazee na baina ya watu wa  mijini na wa mashambani.

Rais wa Ujerumani  pia  amesema  pana haja ya kuleta mageuzi katika  taasisi za  kisiasa ili ziweze kueleweka  na wananchi  na  hivyo  kuweza  kuepusha kutamauka kisiasa  kwa  wananchi wengi na kutokana  na  hayo ametaka kufanyika  kwa  mageuzi  katika mfumo wa kodi  na wa uchaguzi. Katika  hotuba yake ya kila mwaka  kiongozi  huyo  wa Ujerumani amelaumu  jinsi demokrasia inavyotekelezwa  nchini  Ujerumani  na ameshauri kufanyika mabadiliko katika mfumo wa  uchaguzi.