1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Erdogan: Uturuki inaweza kusitisha juhudi za kujiunga na EU

16 Septemba 2023

Rais wa Uturuki Reccip Tayyip Erdogan leo ameashiria kuwa nchi yake inaweza kuachana na mpango wa kijiunga na Umoja wa Ulaya kutokana na kile amekitaja kuwa " mwenendo unaodhihirisha kanda hiyo inaitupa mkono Uturuki".

https://p.dw.com/p/4WQLU
Rais Reccip Tayyip Erdogan wa Uturuki
Rais Reccip Tayyip Erdogan wa Uturuki Picha: AP/dpa/picture alliance

Akizungumza na waandishi habari mjini Istanbul kabla ya kuabiri ndege kuelekea New York kwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Erdogan amesema Umoja wa Ulaya unafanya kila njia kuharibu mahusiano yake na Uturuki.

Alikuwa akijibu swali kuhusu ripoti iliyoidhinishwa na Bunge la Umoja wa Ulaya hivi karibuni ambayo inasema "mchakato wa kuikaribisha Uturuki ndani ya kanda hiyo hauwezi kuendelea chini ya mazingira yaliyopo sasa". Uturuki iliomba kujiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 1999 na mazungumzo yalianza mwaka 2005.

Hata hivyo yalikwama mwaka 2018 baada ya Umoja huo kusema misingi ya kidemokrasia nchini humo imeporomoka.  Jitihada za kuyafufua mazungumzo hayo hadi sasa bado hayajazaa matunda.