1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Ukraine yaishambulia miundombinu ya mafuta ya Urusi

27 Septemba 2025

Urusi imesema droni za Ukraine zimeishambulia miundombinu ya mafuta katika mkoa wake wa Chuvashia. Gavana Oleg Nikolaev amesema mashambulizi hayo yamesababisha mitambo ya mafuta kwenye kituo kilicholengwa kusimama.

https://p.dw.com/p/519Tu
Ukraine imekuwa ikiilenga miundombinu ya mafuta ya Urusi katika wiki za karibuni
Moshi ukifuka katika moja ya mitambo ya mafuta ya Urusi baada ya mashambulizi ya Droni ya UkrainePicha: Veniamin Kondratyev/Telegram/AP Photo/picture alliance

Wakati mashambulii hayo ya Ukraine dhidi ya Urusi yakiarifiwa, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonesha wasiwasi wake kuhusu mashambulizi ya droni yaliyoripotiwa katika mpaka wa nchi yake na Hungary. Kupitia ukurasa wake wa X, Zelensky amesema droni zinazoingia katika anga ya Ukraine zina uwezekano mkubwa kuwa zinatoka Hungary.

Hungary yakanusha droni zake kushambulia Ukraine

Waziri wa mambo ya kigeni wa Hungary Péter Szijjártó, amezijibu tuhuma hizo akisema Zelensky ameanza kuchanganyikiwa na anaanza kuona vitu ambavyo havipo. Ukraine imekuwa ikiikosoa nchi hiyo jirani kwa kile inachokiona kuwa ukaribu na Urusi.