1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Daraja la Baltimore laanguka baada ya kugongwa na meli

26 Machi 2024

Meli moja ya kubeba mizigo imeligonga daraja kuu mjini Baltimore na kusababisha daraja kuanguka. Magari kadhaa yameripotiwa kutumbukia majini na kwa sasa shughuli za uokoaji zinaedelea.

https://p.dw.com/p/4e9Je
USA Baltimore | Einsturz Francis Scott Key Bridge
Daraja kuu la mji wa Baltimore likiwa limedondoka baada ya kugongwa na meli ya mizigoPicha: Julia Nikhinson/REUTERS

Nchini Marekani meli moja ya kubeba mizigo imeligonga daraja kuu kwenye mji wa Baltimore mapema hii leo na kusababisha daraja la Fransis Scott kuangukia mtoni. Magari kadhaa yameripotiwa kutumbukia majini na kwa sasa waokoaji wanaendelea na juhudi  za kuwatafuta watu waliokumbwa na mkasa huo. 

Mapema hii leo kabla ya kuanza kwa shughuli za kawaida,  meli ya mizigo ililigonga daraja hilo kuu la mji wa Baltmore katika jimbo Maryland, chanzo cha meli hiyo ya mizigo kuligonga daraja hilo bado hakijabainika.

USA Baltimore | Einsturz Francis Scott Key Bridge
Muonekano wa daraja la Fransis Scott Key baada ya kuagukia baada ya ajali ya meli ya mizigoPicha: Julia Nikhinson/REUTERS

Afisa mmoja amesema kuwa tukio hilo linaweza kuwa na athari kubwa zaidi kwa sababu ya kutofahamika wazi chanzo cha ajali hiyo, mpaka sasa watu wawili wameokolewa na bado haijulikani ni watu wangapi wanaweza kuwa wapo bado kwenye maji.

 James Wallace,  Mkuu wa shirika la zimamoto wa eneo hilo amesema ''majira ya saa 01:40 asubuhi ya leo,  kituo chetu cha 911 kilituma ujumbe kwa Idara ya Zimamoto ya Jiji la Baltimore kwa ajili ya uokoaji wa maji unaoripotiwa katika Mto PSA katika eneo la daraja kuu. Vitengo vilipokuwa vikijibu, ilianza kupokea simu nyingi zikionyesha watu wengi ndani ya maji. Wakati fulani, wakati huo, msururu huo wa simu, tulianza kupokea dalili kwamba meli imegonga imeligonga  daraja kuu"

Meli hiyo iligonga nguzo moja ya daraja hilo na kusababisha daraja hilo kuanguk majini, picha mbalimbali na video zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari zikionyesha namna daraja hilo lilivyoanguka.

USA Baltimore | Einsturz Francis Scott Key Bridge
Mamlaka zimesimamisha shhughuli zote zab usafirishaji katika eneo hilo baada ya daraja kuu kuangukia mtoniPicha: WJLA/AP/picture alliance

Soma zaidi:  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lashindwa kupitisha azimio la kusitisha mapigano Gaza

Meya wa jiji la Baltmore, Brandon Scott, ameifananisha ajali hiyo na mchezo wa kuigiza.

Mamlaka katika eneo hilo zimesema kwa sasa meli zote za usafirishaji katika eneo la bandari iliyopo jirani na daraja hilo zimesimamishwa ingawa malori yanaruhisiwa kuendelea na shughuli za kawaida.

Itakumbukwa tukio lingine la mwaka 2001, treni ya mizigo iliyobeba vitu vya hatari iliacha njia na kuingia katika moja ya njia ya mji wa Baltmore na kushika moto uliotoa moshi mkubwa. Hali hiyo ilisababisha kufungwa kwa barabara zote kuu za kuingia na kutoka kwenye mji huo.