1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SPD Berlin chagawika kuhusu kuungana na wahafidhina

Iddi Ssessanga
6 Machi 2023

Uamuzi wa meya wa Berlin Franziska Giffey wa kutaka kuongoza serikali ya jimbo hilo pamoja na chama cha Christian Democratic Union CDU, umesababisha mpasuko ndani ya chama chake cha Social Democratic SPD.

https://p.dw.com/p/4OJOB
Wiederholungswahl Berlin - Stimmabgabe Franziska Giffey
Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Hatua ya Giffey ya kupendelea kuunda serikali na chama cha CDU imepingwa na kambi ya chama chake mwenyewe, SPD. Hivi karibuni vyama hivyo viwili vitangaza vitaingia kwenye mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto baada ya CDU kupata ushindi usiokuwa wa kawaida katika uchaguzi wa jimbo hilo mwezi uliopita na chama cha Kansela Olaf Scholz SPD kikaibuka nafasi ya pili.

Giffey kwa sasa anaongoza muungano na vyama vya Kijani na kile cha mrengo mkali wa kushoto cha Die Linke. Hata hivyo uamuzi huo umekigawa chama. Mji wa Berlin ni moja kati ya majimbo 16 yanayounda shirikisho la Ujerumani.

Jumuiya ya wilaya ya Giffey, katika kitongoji cha Berlin kusini ya Neukölln, ilipitisha kwa wingi mdogo hoja ya tawi la vijana la SPD la Jusos siku ya Jumamosi kukataa muungano na CDU, naibu kiongozi wa kundi la chama hicho katika bunge la wilaya Marco Preuß, aliandika kwenye Twitter.