CCM kakanusha madai yaliyotolewa na CUF | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

CCM kakanusha madai yaliyotolewa na CUF

Katibu mkuu wa chama tawala cha CCM huko Tanzania, Yusuf Makamba amekanusha madai yaliyotolewa na mwenyekiti wa chama cha upinzani cha CUF,Profesa Ibrahim Lipumba kwamba CCM hiyo ndio inayosusuwa na kuchelewesha kupatikana ufumbuzi kwenye mazungumzo ya kuuondosha mpasuko wa kisiasa wa visiwani Zanzibar.

Alisema haina haja ya kuwaingiza wapatanishi wa nje kusaidia kuyanusuru mazungumzo hayo yasivunjike, kama inavotakiwa na CUF. Alisisitiza kwamba mazungumzo yanaendelea.

Othman Miraji alizungumza na Bwana Yusuf Makamba.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com