CARACAS: Marekebisho yataimarisha madaraka ya Chavez
3 Novemba 2007Matangazo
Bunge la Venezuela limeidhinisha marekebisho kadhaa katika katiba ya nchi,ambayo yataimarisha madaraka ya Rais Hugo Chavez.Miongoni mwa marekebisho hayo ni kuondoshwa kiwango cha kushika madaraka kwa awamu mbili tu na awamu hiyo sasa inarefushwa kutoka miaka sita kuwa saba na vile vile benki kuu itanyangánywa uhuru wake. Marekebisho hayo yameungwa mkono na wabunge 160 kutoka jumla ya 167.Raia wa Venezuela watapiga kura ya maoni mapema mwezi Desemba.