Bush atoa mwito kuunda serikali ya mseto Kenya | Habari za Ulimwengu | DW | 16.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Bush atoa mwito kuunda serikali ya mseto Kenya

COTONOU:

Rais wa Marekani George W.Bush akiendelea na ziara yake ya siku sita barani Afrika,ameondoka Benin.Kituo chake cha pili ni Tanzania.Wakati wa ziara hiyo mada kuu ni kusisitiza misaada ya Marekani katika ujenzi wa shule,kupiga vita malaria na UKIMWI pamoja na juhudi za nchi hiyo kutenzua migogoro ya Bara Afrika.Alipowasili nchini Benin,Bush alitoa mwito kwa makundi hasimu nchini Kenya kugawana madaraka.Amesema,Kenya ni tatizo na hiyo ni sababu ya kumpeleka waziri wake wa nje Condoleezza Rice nchini Kenya juma lijalo,kusaidia juhudi za Kofi Annan.Amesisitiza kuwa machafuko lazima yasite na yapatikane makubaliano ya kugawana madaraka.

Ziara hii ya siku sita barani Afrika,itampeleka Rais Bush nchini Rwanda,Ghana na Liberia pia.Hadi hivi sasa,Liberia ni nchi pekee iliyo tayari kuiruhusu Marekani katika siku zijazo kuwa na makao makuu ya kikosi kilichoundwa kwa Afrika na kuitwa AFRICOM.Kikosi hicho kiliundwa mwisho wa mwaka jana.Ziara hii inatazamiwa kuwa ya mwisho kufanywa na Rais Bush barani Afrika kabla ya kiongozi huyo kuondoka madarakani Januari mwaka 2009.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com