1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ujerumani kupiga kura ya kupitisha bajeti wiki hii

25 Novemba 2025

Wabunge Ujerumani wiki hii wanatarajiwa kupiga kura ya mwisho kwa bajeti ya mwaka 2026.

https://p.dw.com/p/54E9Y
Deutschland Berlin 2025 | Pressekonferenz nach Koalitionsausschuss mit Söder, Bas, Merz und Klingbeil
Picha: Ralf Hirschberger/AFP

Haya yanafanyika wakati waziri wa fedha Lars Klingbeil akitahadharisha kuwa majadiliano magumu yanatarajiwa katika bajeti za miaka ijayo ya 2027 na 2028.

Klingbeil ambaye ni makamu Kansela na kiongozi wa chama cha Kisoshalisti cha SPD amesema kuwa mpango wake wa rasimu ya fedha kwa miaka baada ya mwaka 2026, una mapungufu makubwa ya ufadhili.

Waziri huyo wa fedha atajadiliana na Kansela Friedrich Merz na mkuu wa chama cha CSU markus Söder baadae mwaka huu.

Katika bajeti hiyo ya mwaka 2026, Ukraine inatarajiwa kupokea kiwango cha rekodi cha yuro bilioni 11.5 kwa ajili ya zana za kivita na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Urusi.

Vyama vya upinzani vimeikosoa pakubwa bajeti hiyo.