1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BREMEN : SPD chajadili mustakbali wa chama

7 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcX

Uongozi wa chama cha Social Demokrat nchini Ujerumani unakutana mjini Bremen kwa siku ya pili kujadili mwelekeo wa sera yake ya kipindi cha usoni.

Mazunguzo juu ya sera za kigeni na masuala ya familia ni miongoni mwa yale yaliomo kwenye agenda.Hapo Jumamosi uongozi wa SPD ulikubaliana juu ya mipango mipya kusaidia wasiokuwa na ajira kwa muda mrefu kupata kazi.

Chama hicho ambacho hivi sasa ni sehemu ya serikali ya mseto ya Muungano Mkuu na chama cha kihafidhina cha Kansela Angela Merkel nchini Ujerumani imekuwa chini ya shinikizo linaloongezeka kutoka kwa wale wanaosema kwamba kinapoteza sifa yake ya kisiasa.