1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOUAKE: Gbagbo aitembelea ngome ya waasi

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdh

Rais Laurent Gbabo wa Ivory Coast ameitembelea ngome ya zamani ya waasi ya Bouake kaskazini mwa nchi hiyo. Ziara ya rais Gbagbo katika eneo hilo ni ya kwanza tangu mapinduzi ya mwaka wa 2002 dhidi ya utawala wake yaliyoigawa Ivory Coast katika eneo la kusini linalotawaliwa na serikali na eneo la kaskazini lililotawaliwa na waasi.

Rais huyo amekuwa mgeni wa heshima kwenye sherehe za upatanisho na kuwapokonya silaha waasi zenye lengo la kuyapa nguvu makubaliano ya amani yaliyosainiwa kati ya serikali na waasi mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bouake rais Gbagbo amesema ana furaha kuona nchi imeungana, jambo ambalo amekuwa akilipigania kwa bidii. Alilakiwa na mwenyeji wake, Guillaume Soro, kiongozi wa zamani wa waasi, aliyeongoza mapinduzi dhidi ya serikali ya rais Gbagbo.

Kwa mujibu wa mkataba wa amani, Soro aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwenye serikali ya umoja wa kitaifa mnamo mwezi Aprili mwaka huu.