1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Borrell aeleza umuhimu wa "mamlaka imara ya Palestina"

26 Mei 2024

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema kuwa "mamlaka imara" ya Palestina ni muhimu ili kupatikane amani katika eneo la Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4gIUr
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep BorrellPicha: Alexandros Michailidis/European Union

Joseph Borrell ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Brussels kabla ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa mamlaka ya Palestina Mohammed Mustafa kuhusu namna utawala wa Palestina unavyoweza kuimarishwa ili kuchukua udhibiti wa Gaza kutoka mikononi mwa kundi la Hamas.

Mwanadiplomasia huyo ameendelea kueleza kuwa, mamlaka imara ya Palestina sio tu muhimu tu kwa Wapalestina bali kwa maslahi ya Israel pia.

Soma pia: Israel yaishambulia Rafah licha ya uamuzi wa ICJ 

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa mamlaka ya Palestina Mohammed Mustafa amesema mkutano wake na Borrell ni fursa muhimu ya kueleza vipaumbele na mipango yao ya baadaye.

Mustafa amesema kipaumbele chao cha kwanza ni kuwaunga mkono Wapalestina katika ukanda wa Gaza kupitia njia ya usitishwaji vita na kisha baadaye kujenga upya taasisi muhimu ndani ya ukanda huo ambao uliingia mikononi mwa Hamas mnamo mwaka 2007.

Israel imekasirishwa na Norway, Uhispania na Ireland kwa kutangaza kuitambua Palestina kama taifa huru.