1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Palestina: Jeshi la Israel limewauwa 7 kwa shambulizi Jenin

21 Mei 2024

Maafisa wa afya wa Palestina wamesema watu wapatao saba wameuliwa katika operesheni ya jeshi la Israel katika mji wa kaskazini wa Ukingo wa Magharibi wa Jenin.

https://p.dw.com/p/4g6A8
Israel, Jenin: Razzia durch israelische Armee in der Westbank
Picha: Zain Jaafar/AFP

Wizara ya afya ya Palestian mjini Ramallah imesema hivi leo kwamba wapalestina tisa wamejeruhiwa, wawili kati yao wakiwa katika hali ya mahututi.

Mkurugenzi wa hospitali mjini Jenin ameiambia televisheni ya Palestina kwamba daktari mmoja ameuliwa kwa risasi akiwa njiani kuelekea kazini.

Kwa mujibu wa wizara ya elimu ya Palestina, mwalimu na mwanafunzi ni miongoni mwa waliouwawa.

Jeshi la Israel limesema limefanya operesheni dhidi ya ugaidi mjini Jenin, mji unaochukuliwa kama ngome ya wanamgambo na unaokabiliwa na uvamizi wa mara kwa mara wa Israel tangu vita vilipozuka Gaza.