1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaishambulia Rafah licha ya uamuzi wa ICJ

25 Mei 2024

Israel imeendeleza hivi leo mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza, ikiwa ni pamoja na mji wa kusini, licha ya uamuzi uliotolewa hapo jana na Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ.

https://p.dw.com/p/4gHAq
Mwanajeshi wa Israel akijiandaa kufyetua risasi huko Rafah
Mwanajeshi wa Israel akijiandaa kufyetua risasi huko RafahPicha: IDF/Xinhua/picture alliance

Mahakama hiyo iliamuru usitishwaji mara moja wa mashambulizi ya kijeshi ya Israel katika mji huo wa kusini wa Rafah.   

Wakati huo huo, juhudi mpya za kidiplomasia zinaendelea mjini Paris ambako rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikutana kwa mazungumzo kuhusu vita vya Gaza na mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa manne ya kiarabu ikiwa ni pamoja na Misri, Jordan, Qatar na Saudi Arabia.

Soma zaidi:Mahakama ya ICJ yaitaka Israel kusitisha mashambulizi huko Rafah

Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Antonio Tajani amesema hii leo kuwa nchi hiyo itaanza tena kulifadhili Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA kwa kutoa sehemu ya kifurushi cha msaada cha dola milioni 38.