1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bishkek:Rais mpya wa Kirgizistan anakiwekea alama ya kuuliza kituo cha kijeshi cha Marekani katika nchi yake

12 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEvE

Rais mpya aliyechaguliwa huko Kirgizistan, Kurmanbek Bakiyev, amesema hana hakika kama Marekani inahitaji kweli kituo cha kijeshi katika nchi yake. Kituo hicho kinatumiwa kama mahala pa kutuwa ndege za Kimarekani zinazofanya operesheni za kijeshi katika Afghanistan. Bwana Bakiyev aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu, Bishkek, kwamba Afghanistan hivi sasa tayari ni tulivu, kwa hivyo sio tena wazi kama Marekani bado inakihitaji kituo hicho kilioko Kirgizistan. Bwana Bakiyev alishinda kwa asilimia 89 ya kura katika uchaguzi wa urais nchini humo jumapili iliopita. Alikuwa anaushikilia wadhifa huo katika kipindi cha mpito tangu mwezi Machi. Huo ni wakati ambapo rais wa zamani, Askar Akayev, aliikimbia nchi baada ya kutokea maandamanao yaliosababishwa na madai kwamba kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi wa bunge.