BERLIN: Shambulio kwenye shule lasababisha kifo cha mshambuliaji na majeruhi kadhaa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Shambulio kwenye shule lasababisha kifo cha mshambuliaji na majeruhi kadhaa

Nchini Ujerumani mtu aliyekuwa na bunduki amepatikana amekufa baada ya kushambulia shule na kuwajeruhi wanafunzi kadhaa na mwalimu wao kwenye shule ilioko Emsdetten karibu na mpaka na Uholanzi. Vifaa vya kuripuwa vimepatikana kwenye mwiili wa mshambuliaji huyo. Polisi haijasema ni vipi mvamizi huyo ambae ni mwanafunzi wa zamani kwenye shule hiyo amekufa. Zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa katika tukio hilo. Wendeshamshtaka wa jamhuri wamesema jana jioni kuwa mvulana huyo wa miaka 18 alikuwa na koromeo 13 za bomu ndogo ya kuripua.

Tukio hilo limekumbusha tukio jingine baya zaidi la mwaka 2002 ambapo mwanafunzi wa zamani aliwauawa wanafunzi 18 kabla ya kujiuwa kwenye shule lake la zamani katika mji wa Erfurt, mashariki mwa Ujerumani.
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com