Belgrade.Ghala ya silaha ya kijeshi yaripuka chini Serbia. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Belgrade.Ghala ya silaha ya kijeshi yaripuka chini Serbia.

Mripuko mkubwa umetokea katika ghala ya silaha ya jeshi la Serbia hii leo, na kuwajeruhi kiasi cha watu 10.

Polisi wamesema mripuko huo umetokea mapema leo katika ghala ya kijeshi karibu na Paracin, kiasi cha kilomita 150 kusini mwa Belgrade, lakini chanzo cha mripuko huo hakijafahamika.

Waziri wa ulinzi wa Serbia Zoran Stankovic amesema ghala hiyo ambayo ilihifadhiwa kiasi kikubwa cha risasi na miripuko imehamishwa baada ya mripuko wa awali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com