BEIJING.Mazungumzo ya pande sita kuendelea leo | Habari za Ulimwengu | DW | 13.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING.Mazungumzo ya pande sita kuendelea leo

Huenda makubaliano yakafikiwa katika mazungumzo ya pande sita juu ya mzozo wa nyuklia wa Korea Kaskazini yanayo endelea mjini Beijing, China.

Wajumbe katika mkutano huo wameeleza kutosheka kwao na mafanikio yaliyopatikana hususan juu ya kutatua pingamizi zilizokabili mazungumzo hayo.

Wajumbe hao wanatarajiwa kukubaliana juu ya mswaada unaotarajiwa kukamilishwa leo hii baada ya mazungmzo hayo kuingia siku yake ya sita.

Baada ya kujadiliana kwa saa 16 mjumbe wa Marekani Christopher Hill aliwaeleza waandishi wa habari kwamba hatua za muhimu zimekwisha fikiwa zinazohusu Korea Kaskazini kuacha mpango wake wa nyuklia.

Lakini mjumbe huyo hakutoa maelezo zaidi.

Mjumbe wa Korea Kusini katika mazungmzo hayo amesema kwamba makubaliano hayo yanahitaji kwanza kupitishwa na serikali za nchi zote zilizowakilishwa katika mazunmgumzo hayo ya pande sita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com