Bei nafuu ya mafuta huenda ikasaidia uchumi | Masuala ya Jamii | DW | 24.11.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Bei nafuu ya mafuta huenda ikasaidia uchumi

Uchumi unapostawi na mahitaji ya mafuta yanapokuwa makubwa,ni wazi kuwa bei ya mafuta itakwenda juu.Ukweli huo ulidhihirika wakati wa majira ya joto,bei ya pipa moja la mafuta ilipofikia Dola 159.

*** Philipp, OPEC bemüht sich, als verlässlicher Partner zu gelten *** ** FILE** Outside view of the headquarters of the Organization of Petroleum Exporting countries (OPEC), on Monday, June 13, 2005, in Vienna. OPEC oil ministers are scheduled to have a meeting in Vienna on upcoming Monday, Sept.11.2006. (AP Photo/Ronald Zak, FILE)

Makao makuu ya shirika la nchi zinazouza mafuta OPEC - yalio Vienna mji mkuu wa Austria.

Lakini sasa si uchumi tu ulioporomoka bali hata bei ya mafuta imeshuka hadi kufikia dola 50 na senti 30 kwa pipa. Bei nafuu ya mafuta inawapa wamiliki makampuni na hata raia wa kawaidia uwezo wa kununua bidhaa hiyo na kwa njia moja au nyingine hiyo husaidia kuchangamsha uchumi.

Bei kubwa za mafuta zimekorofisha ukuaji wa kiuchumi lakini hazijaukwamisha.Sasa mkondo wa mambo ni mwengine.Yaani,kuporomoka kwa bei ya mafuta ni kama kupunguzwa kodi za mapato na kusadia uchumi kwani umma huwa na pesa zaidi mifukoni na hata makampuni pia,lakini hayo yote hayatozuia uchumi kuporomoka.Hata hivyo wafanya biashara na wanunuzi wamefurahi kuona bei ya mafuta ikianguka. Hivi sasa ni kama dola 50 kwa pipa yaani ni theluthi moja ya bei iliyofikia katika majira ya joto.Ikiwa hali ya uchumi itazidi kuwa mbaya basi hata bei ya mafuta itazidi kuporomoka.Lakini kilicho muhimu kwa raia ni kuona kuwa wao pia wanafaidika kwa kupunguziwa bei za petroli,benzin na kadhalika.

Habari nyingine nzuri kwa wateja na hali ya uchumi ni tangzo la mashirika yanayouza gesi kuwa mwanzoni mwa mwaka ujao yatapunguza bei ya gesi. Ni dhahiri kuwa bei ya bidhaa hiyo inaweza kupungzwa kwa zaidi ya asilimia nne hadi saba iliyotangazwa.Kwa hivyo ikilazimika,idara inayosimamia muungano wa wakiritimba iingilie kati,kwani faida inayopatikana kutokana na bei nafuu ya mafuta isibakie kwa wamiliki biashara tu hata wateja wanapaswa kunufaika.Kwani hizo si fedha ndogo.Inakadiriwa kuwa kuanzia kipindi cha majira ya joto hadi mwisho wa mwaka huu,gharama za wateja na wamiliki biashara za kununua mafuta zitapunguka kwa zaidi ya Euro bilioni kumi.Hata ikiwa bei ya mafuta haitoshuka zaidi,lakini bei ya gesi itapunguka kama ile ya mafuta- kwa hivyo mwakani gharama za kulipia bidhaa hizo mbili zitapunguka kwa kama Euro bilioni ishirini.

Lakini kuna upande mwingine wa kuzingatiwa.Kwani nchi zinazoagizia mafuta zinapolipa pesa kidogo,pato la wauza mafuta pia hupunguka. Hatimae Ujerumani inayouza bidhaa zake za viwanda katika nchi za nje itaumia.Isitoshe,nchi zinazouza mafuta huenda zikapunguza uzalishaji ili kuzuia kuanguka zaidi kwa bei ya mafuta na mapato.

 • Tarehe 24.11.2008
 • Mwandishi K.Zawadzky - (P.Martin)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G1Dh
 • Tarehe 24.11.2008
 • Mwandishi K.Zawadzky - (P.Martin)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G1Dh
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com