BAGHDAD: Uturuki imeimarisha vikosi mpakani na Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 09.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Uturuki imeimarisha vikosi mpakani na Iraq

Serikali ya Iraq imevituhumu vikosi vya Uturuki kuwa vinafyatua risasi upande wa pili wa mpaka kaskazini mwa Iraq.Barua ya malalamiko rasmi imewasilishwa kwa balozi wa Uturuki mjini Baghdad.Katika majuma ya hivi karibuni,Uturuki imeimarisha vikosi vyake vya mpakani huku viongozi wa nchi hiyo wakijadiliana ikiwa wawafurushe waasi wa Kikurd wa chama cha PKK wanaopigania kujitenga.Wizara ya mambo ya nje ya Iraq inasema,risasi zilizofyatuliwa na vikosi vya Uturuki,vimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo lililo kati ya Arbil na Dahuk kaskazini mwa Iraq.Jumatano iliyopita,Uturuki ilikanusha madai kuwa vikosi vyake vilivuka mpaka.Wachambuzi wa kisiasa wanasema,Uturuki ina hofu kuwa katika eneo la Kirkuk,lenye utajiri mkubwa wa mafuta kaskazini mwa Iraq na linalodhibitiwa na Wairaqi wenye asili ya Kikurd,huenda likaundwa taifa huru la Wakurd.Marekani iliyo mshirika mkuu wa Uturuki,imeionya serikali ya Ankara kutovamia eneo hilo la mpakani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com